Rombo:wakulima wa zao la kahawa katika wilaya ya rombo
mkoani kilimanjaro wameiomba serikali kutoa ruzuku ya pembejeo ili kufufua zao
la kahawa katika wilaya ya rombo kutokana na wannachi wengi kukata tamaa
kutokana na serikali kutowapa msaada
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema kuwa zao la kahawa
linaiingizia serikali kodi kubwa na pia linaongeza kipato kwa wannachi lakini
kwa muda mrefu serikali imekua ikitoa ruzuku za pembejeo kwa mazao mengine
lakini haitoi kwa wakulima wa zao la kahawa
Mmoja wa wakulima maarufu wa zao hilo wilayani rombo
fredrick silayo amesema kuwa kama serkali ingetoa ruzuku za pembejeo kama vile
madawa wakulima wengi wangelima zao hilo ambalokwa kiasi kikubwa limekua ni
mkombozi kwa wananchi mkoani kilimanjaro
Silayo amesema kuwa wakulima wa zao la kahawa wanakabiliwa
na changamoto nyingine nyingi ikiwemo ukosefu wa elimu ya kutosha na wadudu
kushambuliwa zao hilo pamoja na kuyumba kwa bei mara kwa mara katika masoko
Hapo awali zao la kahawa mkoani kilimanjaro lilikuwa likiwaingizia wananchi kipato kikubwa ambao wakazi wengi mkoani humo wamesomeshwa kwa kipato cha kahawa,kujenga na hata kuinua uchumi wa familia lakini kwa miaka ya hivi karibuni wakulima wengi wamekata tamaa na hata kung'oa mibuni ya kahawa kutokana na kile wanachodai kuwa ni gharama za uzalishaji kuongezeka
Hali hiyo pia imesababisha umasikini katika familia nyingi na hivyo ni vyema serikali ya awamu ya tano kuwaangalia wakulima hao kwa jicho la huruma

EmoticonEmoticon