ROMBO:Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Rombo,evarist silayo amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Rombo akikabiliwa na kosa moja la kumtolea lugha ya matusi mkuu wa wilaya ya Rombo
Akisoma hati ya mashtaka mahakamani hapo mwendesha mashtaka
wa polisi mkaguzi msaidizi bernad machibya,mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama
hiyo,naomi mwerinde amesema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo julai 17 mwaka
huu
”mshtakiwa evarist silayo
bila uhalali mnamo tarehe 17 julai mwaka huu alimtolea lugha ya matusi
agnes elias hokoro ambaye ni mkuu wa wilaya ya Rombo ambapo alimwambia kuwa
acha siasa za kipuuzi,huo ni upumbavu ukiendelea utaondoka kama mwenzio kipuyo”alisema
machibya
Mshtakiwa ambaye pia ni diwani wa kata ya ngoyoni wilayani
Rombo alikana kuhusika na kosa hilo,ambapo mwendesha mashataka wa polisii
aliieleza mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika
Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti
ya dhamana ambapo alitakiwa kuwa n a wadhamini wawili wa kuaminika ambapo
walisaini hati ya shilingi milioni moja na kesi hiyo inatarajiwa kuanza
kusikilizwa masikilizo ya awali septemba 26 mwaka huu
Wakati huo huo mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Ebenezer heromini
woisso(16) mwanafunzi katika shule ya sekondari olele amefikishwa mahkamani
hapo akikabiliwa na makossa mawili,kuzini na maharimu na kumpachika dada yake
ujauzito
Akisoma hati ya mashtaka mahakamani hapo mmwendesha amshtaka
wa polis bernad machibya amedai kuwa mshtakiwa bila uhalali muda na saa
isiyofahamika mwaka huu huko katika kijiji cha kooti mashati mshtakiwa alifanya
mapenzi na dada yake kinyume na sharia na katika shtaka la pili anadaiwa
kumpachika mimba dada yake(14)ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika
shule ya sekondari horombo wilayani humo
Mshtakiwa amekana mashtaka yote na amechiwa kwa dhamana
baada ya kutimiza masharti ya dhamana
EmoticonEmoticon