Have an issue? Contact us 0786733503

Have an issue? Contact us 0786733503

HATIMAYE MADIWANI CHADEMA WAACHIWA KWA DHAMANA

Diwani wa kata ya kingachi Daud mlasani tarimo(kushoto) na makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya rombo Nicolausi Kimario wakishangilia baada ya kuachiwa kwa dhamana(picha na swahili4G)

ROMBO:HATIMAYE Mahakama ya wilaya ya Rombo mkoani kilimanjaro
imewaachia kwa dhamana madiwani watatu wa halmashauri ya wilaya ya
Rombo baada ya kukaa rumande kwa siku saba kutokana na mahakama kuzuia
dhamana kwa washtakiwa hao ambao wanakabiliwa na kesi ya uchochezi
Washatakiwa hao ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya
Rombo,nicolausi kimario ambaye pia ni diwani wa kata ya kirongo
samnaga,Anicia amede diwani wa viti maalumu,daudi mlasani tarimo
diwani kata ya kingachi na mjumbe mmoja wa serikali ya kijiji hendri
kanje wote kupitia chama chademokrasia na maendeleo chadema
Awali wakili anayewatetea washtakiwa Wakili joseph peter aliiomba
mahakama hiyo kuwapa washtakiwa dhamana kwa kuwa kosa wanaloshtakiwa
nalo lina dhamana,ambapo mwendesha mashtka wa polisi inspector bernad
machibya aliiambia mahakama kuwa upande wa mashtka hauna pingamizi juu
ya ombi hilo
Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani  kwa mara ya kwanza tarehe 29
august na kusomewa shtaka moja la uchochezi ambapo inadaiwa kuwa
washtwakiwa hao bila uhalali walifanya mkutano wa ndani na
kuhamasiha wananchi kuichukia mamalak halali ya jamhuri ya muungano
wa Tanzania na serikali yao
Baada ya kuachiwa kwa dhamana wananchi wa tarafa ya useri pamoja na
wafuasi wa chadema waliwapokea madiwani hao ambao wote ni wakazi wa
Usseri kwa maandamano makubwa

Related Posts


EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng
:lv