BODI ya chama cha msingi cha ushirika wa kilimo na mazao makiidi
maharo amcos kimemsimamisha kazi meneja msaidizi wa chama hicho martha kimario
Kwa tuhuma za kuisababishia hasra chama hicho kiasi cha shilingi 985,611
Taarifa hiyo imetolewa na mwenyekiti wa chama hicho Jacobo
kimario jana wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho ambapo amesema kuwa bi
kimario ambaye alikuwa karani na msaidizi wa meneja wa makiidi maharo amcos
alisababisha upotevu wa kiasi hicho cha fedha katika mradi wa duka la pembejeo
la chama chao
Aidha amesema kuwa ajira yake imesitishwa mnamo tarehe machi
15 ambapo amesema kuwa taratibu nyingine zinafuata
Baadhi ya wananachama wa chama hicho wamesema kuwa kumsimamisha kazi haitoshi na
badala yake wafanye uchunguzi wa kina na ikibainika alifanya kosa hilo alipe
fedha zote kwani fedha hizo ni za wanachama wanaouza kahawa zao
Awali akizungumz akatika mkutano huo afisa ushirika wa
halmshauri ya wilaya ya Rombo John Kabataamewataka wananchma wa chama hicho
kujengwa mtajji wao wa ndani ili kuepukana na hali ya utegemezi kwa kukopa
benki na taasisis nyingine za kifedha
EmoticonEmoticon